1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Ujerumani laongeza muda wa jeshi lake dhidi ya IS

11 Novemba 2016

Bunge la Ujerumani limepitisha muswaada wa kuongeza muda wa jeshi lake katika misheni maalum ya kupambana na kundi la Dola la Kiislamu IS kutokea kambi ya Incirlik iliyoko nchini Uturuki.

Deutschland Berlin Innenausschuss
Picha: picture-alliance/dpa/M. Gambarini

Maamuzi hayo awali yalikabiliwa na utata kutokana na mzozo baina ya Ujerumani na Uturuki unaoendelea.

Muswaada huo wa kuliongezea muda jeshi la Ujerumani ambalo linatumia kambi ya Incirlik, nchini Uturuki kwa shughuli za kujazia mafuta ndege zake za kivita ulipitishwa kwa kura 445 dhidi ya kura 139 zilizopinga hatua ya kuongeza muda wa misheni hiyo.

ndege za kivita za Ujerumani aina ya Tornado zinaruka kuelekea  katika operesheni zake kutokea kwenye kituo cha Uturuki cha Incirlik halafu zinapitia Irak kabla ya kwenda Syria huku zikisindikizwa na ndege za kivita za Marekani ambayo inaongoza mapambano hayo dhidi ya kundi la IS.

Jeshi la Ujerumani lina ndege nyingine maalum ya kujaza mafuta kwa ajili ya ndege nyingine za kivita za washirika wake.  Takriban wanajeshi 250 wapo katika kambi hiyo ya kijeshi ya Incirlik.

Mamlaka hayo yanawajumuisha wanajeshi 200 ambao watakuwa  ndani ya manowari ya Ujerumani "Frigate Augsburg" inayosaidia manowari ya Ufaransa ya kubeba ndege ya "Charles de Gaule katika bahari ya Mediterranian. ndege za kivita za Ufaransa zinafanya mashambulizi yake dhidi ya shabaha za  IS kutokea kwenye manowari hiyo.

Hata hivyo wanajseshi wa Ujerumani hawana ruhusa ya kushiriki katika mapigano ya moja kwa moja katika mchango wake wa askari 1200 kwa vikosi washirika. Baadae wanajeshi wa Ujerumani watawajibika pia katika misheni za jumuiya ya kujihami ya NATO. watakuwemo kwenye manowari ya AWAC ambayo itakita karibu na mji wa Konya nchini Uturuki kwa ajili ya kukusanya taarifa za kiintelijensia.  Robo tatu ya wanajeshi ndani ya manowari hiyo ya NATO ni wajerumani.

Manowari ya UjerumaniPicha: AP

Ujerumani ilipeleka vifaa vyake vya kijeshi nchini Uturuki kwa mara ya kwanza mwezi Novemba mwaka 2015 baada ya mashambulio ya kigaidi ya mjini Paris hii ikiwa ni hatua ya kuiunga mkono Ufaransa lakini misheni hiyo imezua maswali mengi hasa baada ya kuongezeka kwa mvutano baina ya nchi mbili za Ujeruamni na Uturuki.

Mvutano waendelea kati ya Ujerumani na Uturuki

Mvutano huo ulisababishwa na hatua ya bunge la Ujerumani kupitisha azimio la mwezi Juni linalotambua mauaji ya jamii ya Waarmenia, Ottoman ya mwaka 1915 huko Uturuki kuwa ni mauaji ya halaiki. baada ya hatua hiyo Uturuki iliwazuia baadhi ya wabunge wa Ujerumani kuingia nchini humo katika safari yao ya kuwatembelea wanajeshi wa Ujerumani walikoko katika kambi ya Incirlik lakini baadae Uturuki ililegeza msimamo wake baada ya serikali ya Berlin kutoa tamko kwamba azimio la mweziJuni halikuwa  mafungamano yoyote.

Mbali na hayo uhusiano wa mataifa haya mawili washirika wa NATO umezidi kuzorota hasa baada ya jaribio la mapinduzi nchini Uturuki lililozimwa la mwezi July. Ujerumani imeendelea kukerwa na misako na kukamatwa watu kunakoendelezwa na mshrika wake Recep Tayyip Erdogan hatua ambayo inaona kuwa ni ukiukaji wa demokrasia.

Kambi ya Incirlik ilihusika sana katika jaribio hilo la kumpindua rais wa Uturuki jambo ambalo lilipelekea kufungwa kwa kambi hiyo kwa muda mfupi huku maswali ya kiusalama yakichomoza. Vile vile Uturuki haipendezwi na taarifa za vyombo vya habari kuhusu matukio ya nchini humo.

Wabunge wa Ujerumani wamesisitiza juu ya kuongezwa muda wa jeshi la Ujerumani kuwa ni hatua ya kuunga mkono vikosi vya kimataifa dhidi ya IS na pia kuilinda Ujerumani dhidi ya mashambulio ya kigaidi na wala sio kuiunga mkono Uturuki.

Chama kikuu chan upinzani cha SPD kilipinga maamuzi hayo kwa sababu za kukatazwa wabunge wa Ujerumani kutembelea kambi ya Incirlik na pia kinahoji juu ya Euro milioni 60 fedha zilizowekezwa katika kambi hiyo.  Vile vile mbunge wa chama cha upinzani cha Kijani Omid Nouripour ameeleza wasiwasi wake juu ya taarifa za kiintelijensia zinazokusanywa na jeshi la Ujerumani  kama hazitotumiwa na Uturuki dhidi wa wapiganaji wa Kikurdi wa nchini Syria.

Mwanzoni serikali ya Ujerumani ilikataza kuipa picha Uturuki zilizoonyesha maeneo ya wapiganaji wa Kikurdi walioko nchini Syria kwa sababu serikali ya Uturuki inawachukulia kuwa ni wafuasi wa kundi la Kurdistan PKK ambalo linaendeleza mapambano dhidi ya serikali ya Ankara.

Mwandishi: Zainab Aziz/DW English

Mhariri:   Yusuf Saumu