Bunge la Ujerumani lapitisha bajeti ya mwaka 2012
26 Novemba 2011Matangazo
Bajeti hiyo ya euro bilioni 306, imepitishwa kwa kura kutoka vyama vya mrengo wa kulia na kati, vya serikali ya mseto ya Kansela Angela Merkel, baada ya siku kadhaa za majadiliano Bungeni. Kiwango cha kukopa kitakuwa kikubwa kidogo, ikilinganishwa na kile cha euro bilioni 22, cha mwaka huu.
Waziri wa Fedha, Wolfgang Schäuble, amesema anatarajia nakisi ya bajeti ya mwaka ujao, itakuwa ya chini kidogo kuliko ya mwaka huu. Upinzani umemlaumu Kansela Merkel kwa kuongeza deni jipya, huku kiongozi huyo wa taifa kubwa kiuchumi Ulaya, akizihubiria serikali nyengine barani humu, kupunguza ukopaji ili kukabiliana na mgogoro wa madeni.
Mwandishi: Mohammed Khelef/ZPR
Mhariri: Prema Martin