1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Ulaya laalani hatua ya kushikiliwa Tundu Lissu

8 Mei 2025

Bunge la Ulaya limeidhinisha Alhamisi maazimio ya haki za binadamu kuhusu Tanzania, na kulaani hatua ya kutiwa nguvuni mwanasiasa Tundu Lissu ambaye ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo Chadema.

Kikao cha Bunge la Ulaya
Bunge la Ulaya katika moja ya vikao vyakePicha: Antonin Utz/SIPA/picture alliance

Katika azimio lao, wabunge wa Ulaya wamelaani kukamatwa kwa kiongozi huyo na kueleza wasiwasi wao mkubwa kuhusiana na tuhuma za kisiasa dhidi yake ambazo hukumu yake huenda ikawa ni kifo.

Tundu Lissu, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema.Picha: Emmanuel Herman/File Photo/REUTERS

Aidha Bunge hilo la Ulaya limezitaka mamlaka za Tanzania kurejesha ushiriki kamili wa  Chadema  katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, kufanya mazungumzo na vyama vyote vya siasa kuhusu mageuzi ya uchaguzi, kuheshimu haki za vyama vya siasa na kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW