1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Li Qiang ateuliwa kuwa waziri mkuu mpya China

11 Machi 2023

Bunge la umma wa China, limemteua Li Qiang kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo,

Li Qiang | China | Shanghai
Picha: Wei Yao/HPIC/picture alliance

Idadi kubwa ya wajumbe takriban elfu 3 ilimpigia kura Li wa umri wa miaka 63 wakati wa mkutano wa wiki moja wa kila mwaka wa bunge hilo, hili likiwa kusanyiko kubwa la chama cha Kikomunsti nchini China. Mwanasiasa huyo mashuhuri anajulikana kuwa mshirika wa karibu wa rais Xi Jinping.

Li, amechukua nafasi ya waziri mkuu anayeondoka Li Keqiang baada ya mihula miwili madarakani. Li Qiang amefanya kazi kwa muda mrefu zaidi katika Pwani ya Mashariki ya China na anasifika kwa utaalamu wa masuala ya kiuchumi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW