1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUbelgiji

Bunge la EU lakaa kimya kuwakumbuka wahanga wa Oktoba 7

8 Oktoba 2024

Wabunge wa Umoja wa Ulaya jana Jumatatu walikaa kimya kwa dakika moja ili kuwakumbuka wahanga wa shambulio la Oktoba 7 lililofanywa na kundi la Hamas dhidi ya Israel.

Brüssels | Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya | Ursula von der Leyen
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der LeyenPicha: Nicolas Economou/NurPhoto/picture alliance

Wabunge wa Umoja wa Ulaya jana Jumatatu walikaa kimya kwa dakika moja ili kuwakumbuka wahanga wa shambulio la Oktoba 7 lililofanywa na kundi la Hamas dhidi ya Israel huku Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen akiapa kupambana na chuki dhidi ya Wayahudi.

Von der Leyen amekosoa kile alichokitaja kama ongezeko la kutisha la chuki dhidi ya Wayahudi barani Ulaya wakati alipohudhuria hafla ya kumbukumbu ya shambulio la Oktoba 7 iliofanyika mjini Brussels.

Soma pia:  Von der Leyen aizuru Ukraine kujadili usalama wa nishati

Amesema kuwa chuki dhidi ya Wayahudi ni tishio kwa demokrasia na kufananisha chuki hiyo kama saratani inayotishia misingi ya Umoja wa Ulaya.

Kulingana na takwimu za shirika la habari la AFP, shambulio la Hamas katika ardhi ya Israel lilisababisha vifo vya watu 1,205 wengi wao wakiwa raia.

Maadhimisho ya kumbukumbu ya shambulio la Oktoba 7 yamefanyika wakati Israel inaendeleza oparesheni ya kijeshi katika ukanda wa Gaza na kwa upande mwengine, jeshi la nchi hiyo linapambana na kundi la Hezbollah nchini Lebanon.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW