1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Urusi na mzozo wa Caucasus

Hamidou, Oumilkher26 Agosti 2008

Eti kweli Urusi yataka mvutano na Magharibi?

Rais Dmitri Medvedev wa UrusiPicha: AP



Mwito wa bunge la Urusi kuitaka serikali ya mjini Moscow iyatambue majimbo ya Georgia yaliyojitenga-Abkhasia na Ossetia ya kusini ndio mada iliyohodhi magazetini hii leo.Wahariri wamechambua  pia utafiti uliofanywa na taasisi ya Ujerumani ya huduma za uzeeni  kuhusu bima ya malipo ya uzeeni.


Kuhusu hali namna ilivyo katika eneo la Caucasus,gazeti la LEIPZIGER VOLKSZEITUNG linaandika:



"Jinsi baraza la majimbo ya shirikisho la Urusi na bunge la Duma yanavyozungumzia Ossetia ya kusini na Abkhasia zitambuliwe kama nchi huru,utadhani hakuna makubaliano ya vifungu sita yaliyoshauriwa na Umoja wa ulaya na kutiwa saini na Urusi! Muda mfupi tuu baada ya mkutano wa dharura wa viongozi wa Umoja wa ulaya kuhusu mzozo wa Georgia kumalizika,Moscow iliwalaghai viongozi hao na kuendelea kutuma vifaru vyake katika eneo hilo.Hata kama rais Medvedev  hajaitika bado mwito  huo wa bunge,hata hivyo kura iliyoipigwa bungeni anaweza kuitumia kama turufu katika meza ya mazungumzo."



Gazeti la BADISCHE ZEITUNG la mjini FREIBURG linahisi:


"Tuchukulie kwamba wabunge hawakupitisha uamuzi huo kwa khiari yao,pengine wameshawishiwa na rais Medvedev au hata pengine kuamriwa na mkubwa wake wa kichini chini,Putin.Viongozi wa Urusi wanataka kuutumia mshutuko uliopiga nchini kwa masilahi yao na wanataka kuwachochea wazungu na wamarekani pia.Wanahisi wana nguvu za kutosha kuweza kukusanya hoja za kila aina ili kujitoa baadae kifua mbele pindi udhalimu wao ukishindikana.



Gazeti la THÜRINGER ALLGEMEINEN la mjini Erfurt linaamini:


"Bado kuna matumaini ya kumuona rais Medvedew akikwepa mvutano pamoja na nchi za magharibi na kupinga kwa hivyo mwito wa wabunge.Suala linalozuka ni jee ana weza kufanya hivyo na jee anataka kweli?Hakuna atakaemuelewa nchini Urusi.Atajikuta peke yake kwasababu,msimamo wa mabaraza yote mawili ya bunge,unaonyesha kuungwa mkono sio tuu na wafuasi wa Putin katika ikulu ya Kremlin, bali hata na jeshi na wananchi pia.



Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG linatafsiri ifuatavyo msimamo wa Urusi na kuandika:


"Kuirejeshea Urusi hadhi yake kama dola kuu ni muhimu zaidi kwa uongozi wa mjini Moscow kuliko kuendeleza ushirikiano wa kimkakati.Rais Medvedev aliwahi kusema wakati mmoja"jumuia ya kujihami ya magharibni NATO ndio yenye kupendelea zaidi ushirikiano pamoja na Urusi.Ni kweli.Si NATO na wala si Umoja wa ulaya,hakuna bado aliyebuni mkakati wa kuweza kukabiliana na Urusi pindi ikianzisha upya sera zake za uchokozi bila ya kujali mazungumzo ya amani.Kwa mara nyengine tena viongozi wa Umoja wa ulaya hawatakua na kazi rahisi kusaka msimamo wa aina moja watakapokutana kwa kikao cha dharura.







Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW