Uturuki lapigia kura ombi la Finnland kujiunga na NATO
30 Machi 2023Matangazo
Bunge la Uturuki linapiga kura mchana huu kuhusu ombi la nchi hiyo ya UIaya Kaskazini kuwa mwanachama wa 31 wa NATO.
Hii ni baada ya Rais Recep Tayyip Erdogan kuhitimisha miezi ya mazungumzo na kulibariki ombi la Finland mapema mwezi huu.
Uturuki yapanga kuidhinisha ombi la Finland kujiunga na NATO
Erdogan analidhibiti bunge kupitia muungano na chama cha siasa za mrengo wa kulia. Wabunge wengi wa upinzani pia wanaunga mkono ombi la Finland.
Idhini ya Uturuki itaiacha Finland, ambayo inapakana na Urusi, na hatua chache tu za kiufundi kabla ya kujiunga rasmi na NATO.