1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUswidi

Bunge la Uturuki laidhinisha ombi la Uswidi kujiunga na NATO

24 Januari 2024

Wabunge wa Uturuki wameidhinisha ombi la Uswidi la kujiunga na jumuiya ya kujihami ya NATO katika kura iliyocheleweshwa kwa muda mrefu na kufungua njia kwa taifa hilo la Nordic kuelekea kupata uwanachama wa NATO.

Waziri Mkuu wa Uswidi Ulf Kristersson
Waziri Mkuu wa Uswidi Ulf KristerssonPicha: Ninni Andersson/Government Offices of Sweden/Xinhua/picture alliance

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anatarajiwa kutia saini na kuafiki uamuzi huo wa bunge ndani ya siku chache zijazo.

Waziri Mkuu wa Uswidi Ulf Kristersson ameandika katika mtandao wa kijamii wa X, kwamba wako hatua moja karibu na kuwa mwanachama kamili wa NATO.

Uamuzi wa bunge la Uturuki kunaiacha Hungary kuwa mwanachama pekee wa NATO ambaye bado hajaidhinisha ombi la Uswidi kupewa uwanachama ndani ya jumuiya hiyo ya kujihami.

Uswidi ilituma maombi ya kutaka kujiunga na NATO mwaka 2022 baada ya Urusi kuivamia Ukraine lakini Uturuki ilikataa kuidhinisha ombi lao kutokana na kile ilichosema nchi hiyo inayawaunga mkono makundi ambayo Ankara imeyaorodesha kama ya kigaidi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW