1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burhan aapa kuvimaliza vita muda mfupi ujao

28 Agosti 2023

Kiongozi wa jeshi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, amesema muda umefika wa kuumaliza uasi wa wanamgambo wa Kikosi cha Dharura (RSF) akiahidi ushindi wa haraka, ikiwa ni miezi minne ya vita vikali nchini humo.

Krieg im Sudan | General Abdel Fattah al-Burhan
Picha: Sudanese Army/AFP

Burhan alisema siku ya Jumatatu (Agosti 28) akiwa katika mji wa Port Sudan kwamba hakuna aliyemsaidia kutoka kwenye makao makuu ya jeshi na wala haikutokana na makubaliano yoyote, bali ilikuwa ni operesheni ya kijeshi yenye mafanikio.

Soma zaidi: RSF iko tayari kuweka silaha chini na kufanya mazungumzo na jeshi la Sudan

Alisema wanahamasisha kila mahali kuuangusha uasi huo uliofanywa na mamluki wanaotoka maeneo mbalimbali ulimwenguni.

"Hakuna tena muda wa majadiliano, bali kwa sasa tunaelekeza nguvu zote kwenye vita ili kuuhitimisha uasi huu," alisema jenerali huyo kwenye ziara yake ya kwanza nje ya makao makuu ya jeshi tangu mwezi Aprili yalipoanza mapigano.

Burhan alitoa matamshi hayo siku moja baada ya kiongozi wa RSF, Mohamed Hamdan Dagalo, kuchapisha taarifa yenye mapendekezo 10 ya kuvimaliza vita na kujenga kile alichokiita "Sudan Mpya."
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW