Burhan asema vita havitokwisha Sudan hadi RSF wasalimu amri
30 Machi 2025
Katika hotuba yake ya kwanza tangu jeshi lake lilipochukua udhibiti wa mji Mkuu Khartoum, Al Burhan amesema mwisho wa vita vya takriban miaka miwili kati ya pande hizo mbili hasimu utawezekana tu iwapo kundi hilo litaweka chini silaha zake.
Kiongozi huyo wa kijeshi ameondoa uwekekano wa mazungumzo kati ya pande hizo mbili akiapa kupambana nao hadi mwisho.
"Kwa watu wa Sudan, njia ya amani na kumaliza vita bado iko wazi. Kuteseka kwa watu wetu katika maeneo yanayoshikiliwa na wanamgambo, kuzingirwa kwao, kuuwawa na uharibifu hasa katika eneo la El Fasher, na umuhimu wa kueneza amani na uthabiti katika nchi hii...Haya yote yanawezekana na njia iko wazi. ni lazima wanamgambo waweke chini silaha zao," alisema al Burhan.
Jeshi la Sudan lasema limerejesha udhibiti wa mji mkuu
Hotuba ya Burhan imekuja siku kadhaa kuidhibiti Ikulu ya rais iliyokuwa chini ya RSF tangua kuanza kwa vita hivyo takrioban miaka miwili iliyopita. Hata hivyo kiongozi wa wanamgambo hao Mohammed Hamdan Dagalo amesema kamwe hawatosalimu amri.