1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burhan asema yuko tayari kuzungumza na Trump kuhusu amani

16 Desemba 2025

Kiongozi wa Kijeshi nchini Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, yuko tayari kufanya kazi na Rais wa Marekani Donald Trump kutatua mzozo unaoigawanya nchi yake. Haya yamesemwa leo na wizara ya mambo ya nje.

Sudan Khartum 2025 | Burhan
Kiongozi wa jeshi nchini Sudan, Abdel Fattah al-Burhan akiwapongea mkono wanajeshi baada ya kuchukuwa udhibiti wa Khartoum mnamo Machi 26, 2025Picha: Sudan Transitional Sovereignty Council/Handout via REUTERS

Wizara hiyo ilitoa taarifa baada ya Burhan kufanya ziara mjini Riyadh kama mgeni wa Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman, ambaye hivi karibuni aliwasilisha kwa Trump mpango wa amani kwa Sudan wakati wa ziara yake Washington.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Burhan alipongeza "kujitolea kwa Trump kushiriki katika juhudi za kufikia amani na kumaliza vita nchini humo, kwa ushiriki wa Ufalme wa Saudi Arabia."

Taarifa hiyo pia imesema Burhan alithibitisha ari ya Sudan kufanya kazi na Rais Trump, waziri wake wa mambo ya nje Marco Rubio, na mjumbe wake wa amani nchini Sudan Massad Boulos ili kufikia lengo hilo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW