1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaBurkina Faso

Burkina Faso kuanzisha kampeni ya chanjo dhidi ya Malaria

6 Februari 2024

Burkina Faso imeanzisha kampeni ya chanjo dhidi ya malaria, wiki mbili baada ya Cameroon kuchukua pia hatua kama hiyo.

Cameroon | Mpango wa Chanjo dhidi ya Malaria
Muuguzi akijiandaa kutoa chanjo ya malaria kwa mtoto mchanga katika kituo cha afya huko Datcheka, Cameroon, Januari 22, 2024. Picha: Desire Danga Essigue/REUTERS

Ugonjwa huo bado ni sababu kuu ya vifo vya watoto wachanga katika nchi hiyo ambayo huorodhesha visa zaidi ya milioni kumi kwa mwaka.

Akiwa Magharibi mwa nchi hiyo katika mji wa Koudougou kulikozinduliwa kampeni hiyo, Waziri wa Afya wa Burkina Faso Lucien Marie Robert Kargougou ameitaja siku ya jana kuwa ya kihistoria kutokana na kile alichosema kuwa chanjo hiyo ni kinga thabiti dhidi ya malaria.

Soma pia: Chanjo ya malaria inafanya vizuri Afrika

Waziri huyo amesema jumla ya dozi 200,000 za chanjo ya RTS,S kati ya dozi 800,000 zinazotarajiwa mwaka huu, zitatolewa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano katika wilaya 27, na kwamba chanjo hiyo itasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa visa vya malaria na idadi ya vifo kutokana na ugonjwa huo.

Utoaji chanjo ya Malaria washika kasi Cameroon

02:11

This browser does not support the video element.