Burkina Faso yaishutumu France 24 'kuwasaidia magaidi'
28 Machi 2023Matangazo
Utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso jana (Machi 27) ulitangaza kusitisha matangazo ya kituo cha televisheni cha France 24, baada ya kituo hicho cha Ufaransa kurusha hewani mahojiano kilichoyafanya na kiongozi wa kundi la Al-Qaeda tawi la Afrika Kaskazini.
Msemaji wa utawala huo wa Burkina Faso, Jean Emmanuel Ouedraogo, amedai kwamba France 24 sio tu ni shirika la mawasiliano kwa ajili ya magaidi hao lakini pia linatoa uhalali wa vitendo vya magaidi na kauli za chuki.
Kituo hicho cha habari kilimuhoji kiongozi wa kundi la kigaidi la AQIM, Abu Ubayda Yusuf al-Annabi.
Ouedraogo amesema wanaamini mahojiano hayo yaliyorushwa hewani ni sehemu ya mchakato wa kuhalalisha ujumbe wa magaidi na wanafahamu kuhusu athari za ujumbe huo nchini Mali.