1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurkina Faso

Burkina Faso yapokea ngano iliyoahidiwa na Urusi

27 Januari 2024

Burkina Faso imepokea tani 25,000 za ngano bila malipo iliyoahidiwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin kama sehemu ya msaada kwa mataifa sita ya Afrika

Uvunaji ngano katika kijiji cha Zgurivka eneo la Kyiv nchini Urusi mnamo Agosti 9, 2022
Uvunaji ngano katika eneo la Kyiv nchini UrusiPicha: picture alliance / NurPhoto

Nafaka hiyo ilikuwa imeahidiwa na Putin wakati wa mkutano wa kilele wa Urusi na mataifa hayo ya Afrika yanayozijumuisha Mali, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Eritrea, Somalia na Zambia mjini Saint Petersburg mnamo Julai mwaka jana.

Burkina Faso yasifu hatua ya Urusi ya kupeleka ngano nchini humo

Waziri wa mshikamano na hatua za kibinadamu wa Burkina Faso Nandy Some Diallo, amesema ngano hiyo imeonesha kujitolea kwa Urusi katika kuunga mkono juhudi za mamlaka ya nchi hiyo inayokabiliwa na mzozo wa usalama.

Soma pia:Putin akutana na viongozi wa Afrika

Balozi wa Urusi Alexei Saltykov, amesema ngano hiyo ni ishara kali ya nia ya rais wake ya kutoa msukumo mkubwa kwa ushirikiano na Burkina Faso, mmoja wa washirika wake wa kimkakati barani Afrika.

Soma pia:Putin aipongeza Afrika inavyoshughulikia masuala ya kimataifa

Waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso Karamoko Jean Marie Traore amesema msaada huo unapaswa kusaidia kuishinikiza nchi hiyo kuimarisha uwezo wake wa uzalishaji chakula ili kukomesha mara moja utegemezi wa chakula kutoka nje.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW