1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurundi

Burundi: Mkuu wa ujasusi akamatwa kwa kuvujisha taarifa

18 Aprili 2023

Taarifa kutoka nchini Burundi zinabaini kuwa Mkuu wa idara ya Ujasusi wa nje Alfred Innocent Museremu pamoja na Mkuu wa kitengo cha polisi wa kutuliza ghasia Désiré Uwamahoro wamekamatwa

Burundi | Besuch Premierminister | Alain Guillaume Bunyoni
Picha: Antéditeste Niragira/DW

Taarifa kutoka nchini Burundi zinabaini kuwa Mkuu wa idara ya Ujasusi wa nje Alfred Innocent Museremu pamoja na Mkuu wa kitengo cha polisi wa kutuliza ghasia Désiré Uwamahoro wamekamatwa.

Wawili hao wanatuhumiwa na mamlaka kwa kutoa taarifa kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Alain Guillaume Bunyoni kuhusu msako uliyopangwa kufanyika nyumbani kwake hapo jana.

Vyombo kadhaa vya habari vimebaini kuwa kwa sasa Bunyoni ameondoka Burundi na huenda tayari amewasili nchini Tanzania. Alain Guillaume Bunyoni ni mwanachama wa chama tawala Cndd Fdd

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW