1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurundi

Burundi yadai Rwanda inawasaidia waasi

12 Mei 2024

Burundi imeituhumu Rwanda kwa kuwapa mafunzo na silaha waasi wanaolaumiwa kwa mashambulizi mawili ya guruneti ambayo yalisababisha kujeruhiwa kwa watu 38 siku ya Ijumaa

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye akizungumza wakati wa kongamano la COP28 mjini Dubai mnamo Desemba 2,2023
Rais wa Burundi Evariste NdayishimiyePicha: Rafiq Maqbool/AP/picture alliance

Wizara ya mambo ya ndani imesema kuwa waasi wa kundi la RED-Tabara wanaoshutumiwa kwa msururu wa mashambulizi nchini Burundi kwa usaidizi waRwanda, walirusha guruneti kwenye kituo cha mabasi kilichokuwa kimejaa watu katika mji mkuu Bujumbura siku ya Ijumaa jioni.

Soma pia:Watu 8 wauawa, kadhaa wajeruhiwa Burundi

Msemaji wa wizara hiyo Pierre Nkurikiye amethibitisha kujeruhiwa kwa watu hao 38 na kusema hakuna vifo vilivyoripotiwa, lakini duru za polisi na mashuhuda zimeliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba watu watatu waliuawa.

Burundi imekuwa ikiishtumu Rwanda kwa kuwafadhili waasi

Katika shambulio sambamba na hilo karibu na kituo cha mafuta wilayani Ngagara, Nkurikiye amesema ni mshambuliaji pekee aliyejeruhiwa na kukamatwa. Mara kwa mara, Burundi imekuwa ikiishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi hao, madai ambayo yamekanushwa na serikali ya Rwanda na kundi hilo la RED-Tabara.