1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burundi yafunga mipaka yake na DRC, M23 yauteka Uvira

10 Desemba 2025

Burundi imeifunga mipaka yake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya waasi wa M23 kuingia katika mji wa kimkakati wa Uvira, ulio karibu na mji wa kiuchumi wa Burundi, Bujumbura.

DR Kongo Uvira 2025 | Waasi wa M23 wauteka mji wa Uvira
Burundi yafunga mipaka yake na DRC baada ya M23 kuuteka mji wa Uvira Picha: AFP

Afisa wa jeshi la Burundi amesema, mipaka ya Gatumba na Vugizo imefungwa na inatizamwa kama maeneo yaliyo na shughuli zakijeshi.

Burundi inaiunga mkono serikali ya Kongo katika vita vyake na waasi wa M23 ambao wanadaiwa kuungwa mkono na Rwanda, jambo ambalo Rwanda imeendelea kukanusha.

Maelfu ya raia wa Kongo wamelazimika kukimbilia nchi hiyo jirani ya Burundi baada ya waasi hao kuingia Uvira.

Haya yanatokea licha ya Marekani na mataifa kadhaa ya Ulaya kuwahimiza waasi wa M23, kusimamisha mara moja mashambulizi yao na kuitaka Rwanda kuwaondoa wanajeshi wake kutoka kwenye eneo hilo la mashariki mwa DRC, lenye utajiri mkubwa wa madini.