SiasaBurundi
Burundi yamchagua mpatanishi wa kitaifa
17 Novemba 2022Matangazo
Bunge nchini Burundi limemchaguwa Bi Aimée Lorentine Kanyana kuwa mpatanishi wa kitaifa. Jumla ya wabunge 120 walioshiriki uchaguzi huo, 109 wamepiga kura kuchaguwa mmoja kati ya wagombea 13 wa nafasi hiyo ya mpatanishi wa Warundi. Aimée Lorentine Kanyana, aliyewahi kuwa waziri wa sheria wa Burundi, ni mtu wa tatu kushikilia nafasi hiyo, baada ya Hayati Mohammed Rukara na Édouard Nduwimana ambaye muhula wake umefikia ukingoni. Taasisi ya mpatanishi wa kitaifa ilianzishwa na Mkataba wa Amani uliosainiwa Agosti 28 mwaka 2020 jijini Arusha, Tanzania, chini ya usuluhishi wa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.