1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBurundi

Burundi yaongeza juhudi kutokomeza ujinga

Amida Issa8 Septemba 2023

Burundi imepiga hatua katika kuhakikisha raia wake wanajuwa kusoma na kuandika. Ripoti ya mwaka 2016 ya taasisi ya kitaifa inayohusika na takwimu ISTEBU ilionesha kuwa asilimia 62 ya raia hawajuwi kusoma wala kuandika.

Nigeria DW Reporterin Clara Cheila Dushime im Einsatz
Picha: Antéditeste Niragira/DW

Juhudi kubwa zinafanyika ambapo serikali ilibuni mfumo wa elimu ya msingi unao ishia darasa la 9 ili kuhakikisha watu wote wanajuwa kusoma na kuandika, ingawa bado hakujatolewa takwimu mpya kuonyesha mabadiliko hayo.

Tarafani Musigati katika mkoa wa Bubanza magharibi mwa Burundi, Waziri anaye husika na mshikamano wa kitaifa Imelde Sabushimike akipeleka msaada wa vyakula na vifaa vya shule kwa familia 5225 masikini zaidi. Asilimia kubwa ya familia hizo ni kutoka jamii ya Watwa.

Kujuwa kusoma na kuandika kunapewa kipaumbele na serikali, alisema waziri Sabushimike na kwamba hii ndio sababu serikali imekuwa ikifanya hivyo kila  mwaka wa masomo unapo karibia kuanza,  katika dhamira ya kuwapa moyo wa kukabiliana na umasikini na vile vile  kuhakikisha watoto wanapelekwa shule  kuepukana na ujinga :

" Mnaona shehena ya misaada nilowaletea, pale kuna mchele, kuna maharagwe, na kuna mabati. Na zipo pia daftari. Nilitaka niwambiye kuwa katika vyote, kilicho na thamani kubwa ni daftari. Mwatakiwa kuwapeka watoto shule, ili waondokane na ujinga na waandae maisha yao ya baadaye."

Rais wa Burundi Evariste NdayishimiyePicha: Bujumbura Amida Issa/DW

Ripoti ya karibuni ya taasisi inayo husika na takwimu, ilichapishwa mwaka 2016 inabaini kuwepo na asilimia 62 za warundi wasojuwa kusoma na kuandika. Na asilimia kubwa ya raia hao ni kutoka jamii ya Watwa.

Mbunge Come Manirakiza ambaye amekuwa akijihusisha na kuwasidia raia wenye kipato duni kubuni njia na taratibu za kujiendeleza, anasema ulimwengu ulipo fikia sasa, kusoma na kuandika peke hakutoshi:

" Kuna jukumu la kila mmoja ili kuona anapiga hatua mbele, kwenda shule ni muhimu lakini kuyaendeleza masomo hadi kukamilisha ni muhimu zaidi. Kuna wengi wanaacha shule. Ndiyo sababu kila anaye pata fursa ya kwenda shule anatakiwa kusoma. Kesho Huwezi kuwa mkuu wa kijiji, au wa Tarafa ama mkuu wa mkoa pasina kujuwa kusoma na kuandika. Ndio sababu mnahimizwa wazazi kuwapeleka watoto wenu shule na kuhakikisha wanaendelea na masomo."

Soma piaSiku ya kimataifa ya kupambana na kutokujua kuandika na kusoma nchini Burundi

Jean Marie Ndayisenga Muhadhiri kwenye chuo kikuu cha Burundi anasema licha ya kiwango cha wasojuwa kusoma na kuandika kupunguwa nchini, bado kuna changamoto:

" Miaka miwili imepita tangu kufutwa idara ilokuwa ikifuatilia  raia wote ili waweze kujuwa kusoma na kuandika, na husuan watu wazima. Na kubuniwa mfumo wa elimu unao ishia darasa la 9 ili hadi mwaka 2030 watu wote wawe wanajuwa kusoma na kuandika. Lakini safari bado imesalia ndefu. Na changamoto bado ni nyingi kuna  wale wanao acha shule kwa sababu za umasikini, mimba za mapema. Sisi kama wataalamu tunaona kuwa kuna hitajika juhudi zaidi kwa serikali na wazazi ili kukabiliana na changamoto hizo, kwani mtu asiye juwa kusoma na kuandika ni vigumu kuiendeleza jamii na hata nchi yake."

Hatua iliyoazimiwa na serikali mnamo mwaka 2005, ya kuruhusu elimu ya msingi kutolewa pasina malipo ilipelekea idadi ya wasojuwa kusoma na kuandika kupungua kwa kiasi kikubwa nchini Burundi.

(DW)

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW