1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burundi yapewa nafasi ya uwenyekiti AU

16 Februari 2026

Kuteuliwa Burundi kuwa mwenyekiti wa umoja wa Afrika kunatarajiwa kuleta tija katika kutatuwa migogoro inayo zikabili baadhi ya nchi za jumuia hiyo kutokana na Burundi kuwa na uzoefu katika maswala ya kusimamia amani na

Vereinigte Arabische Emirate | Präsident von Burundi Evariste Ndayishimiye
Picha: Rafiq Maqbool/AP/picture alliance

Burundi kukalia kwa mara yake ya kwanza uwenye kiti wa Umoja wa Afrika kumetathminiwa kama kutaleta manufaa makubwa ndani ya nchi. Rais Evariste Ndayishimiye amesema licha ya kuwepo na changamoto anaimani Burundi itafanikisha majukumu iliyokabidhiwa kwa kuwashrikisha wadau wote, na kumtaka kila Mrundi kuwa mfano mzuri katika ushirikiano.

Profesa Desire Nizigimana Mhadhiri kwenye chuo kikuu cha Burundi na mtaalam alobobea katika maswala ya kimataifa anasema Burundi inao nafasi ya kimkakati, baada ya kabiliwa na migogoro katika miaka ilopita, imekuwa katika msatari wa mbele kuzisaidi nchi nyingine katika juhudi za kusimamia amani na usalama.

Mtaalam Désiré Nisigimana amesema ni kwa maantiki hiyo Burundi iliwapeleka wanajeshi wake katika nchi kama Somalia, Jamuhuri ya Afrika ya kati, Sudan Na jamuhuria ya kidemokrasi ya Congo.

"Burundi ni nchi yenye uzoefu katika kuzisindikiza nchi nyinge kwenye juhudi za kusimamia amani na usalama. Mnakumbuka Burundi iliwatuwa wanajeshi wake Somalia, Jamuhuri ya Afrika ya kati, Sudan Na jamuhuria ya kidemokrasi ya Congo. Burundi kukalia uwenye kiti wa umoja wa Afrika fursa kutamarisha uzowefu wake huo."

Burundi yasema kipaumbele chake ni kurejesha amani barani Afrika

Kwa upande wake mtaalam wa maswala ya kiuchumi Diomede Niterese amesema mwaka 2026 kutapigwa hatua kubwa katika maendeleo yanayo kusudiwa na nchi nyingi za bara la Afrika.

Picha: Eskinder Firew/DW

Naye Mwalimu Diomede Niteretse amesema fursa nyingi zitafunguliwa kwa wawekezaji na uagizaji huria unafaa kuzingatiwa ili lengo hilo liweze kukamilka.

"Mchakato wa maendeleo hufanikiwa ikiwa utakuwa pamoja na wengine, wawekezaji wa Burundi wanatakiwa kuimarisha ushirikiano wao na wale kutoka nchi nyingine miradi ya maendeleo iliyopo Afrika iweze kukamilika."

Rais Evariste Ndayishimiye amesema licha ya kuwepo na changamoto kipa umbele kitawekwa katika kurejesha amani pale ilipo tatizika, kuhakikisha maji safi yanapatikana hadi vijiji vya mbali vya nchi za bara hilo, na ushirikiano uloimarika katika ubadilishaji biashara.

"Tunayakini kuwa majukumu tulokabidhiwa si rahisi, Burundi kubeba bendera ya Afrika kote duniani, na kuwa kiunganisho kati ya nchi wanachama wa umoja wa Afrika. Lakini tulipoazimia kuwepo na Umoja wa Afrika hivyo basi lazima sote tuwe kitu kimoja. Mnajuwa bado kuna maeneo amani na usalama bado vimetatizika lazima tusaidizane sote ili amani na usalama virejeye katika maeneo hayo, mka isiyo na mbadala ni ile ya mazungumzo."

Wamiliki wa Hoteli, migahawa na sehemu nyingine za starehe na kitalii wametakiwa kuboresha mazingira ya kazi kwa sababu wageni wengi wataitembelea Burundi katika mwaka huu wa 2026.

Viongozi wa kikanda wajadili amani ya DRC Uganda

02:10

This browser does not support the video element.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW