1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBurundi

Burundi yatangaza mlipuko wa polio

17 Machi 2023

Burundi imetangaza mripuko wa polio baada ya kugundua visa vya kwanza vya kirusi hicho katika kipindi cha zaidi ya miongo mitatu.

Poliovirus Animation
Picha: StockTrek Images/IMAGO

Maafisa wa afya Burundi waligundua kisa kimoja katika mvulana mmoja mwenye umri wa miaka minne ambaye hajachanjwa, kusini mwa nchi hiyo, pamoja na watoto wengine wawili ambao walikuwa karibu naye.

Sampuli nyingine mbili za kirusi hicho ziligundulika katika majitaka. Polio ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na kirusi ambacho kinauambukiza mfumo wa neva na unaweza kusababisha kupooza kusikoweza kurekebishwa.

Picha ikimuonyesha mtoto anayeugua maradhi ya polio nchini India.Picha: Anindito Mukherjee/dpa/picture alliance

Mamlaka ya afya nchini Burundi imegundua kisa cha mvulana wa miaka minne magharibi mwa nchi hiyo, ambaye hajachanjwa, pamoja na watoto wengine wawili ambao wamewasiliana naye. Shirika la Afya Duniani limeongeza kuwa, sampuli nyingine tano za aina ya polio ya aina ya pili, zilipatikana katika maji machafu.

Polio ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vinavyoambukiza mfumo wa neva na vinaweza kusababisha kupooza bila kurekebishika. Inawadhuru zaidi watoto wadogo, lakini inaweza kuzuiwa kwa chanjo yenye ufanisi na nafuu sana.

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani WHO kanda ya Afrika, Matshidiso Moeti, amesema katika taarifa yake kwamba ugunduzi wa haraka wa visa nchini Burundi unaonyesha ufanisi wa ufuatiliaji wa magonjwa nchini humo.

"Tunaunga mkono juhudi za kitaifa za kuongeza chanjo ya polio ili kuhakikisha kuwa hakuna mtoto anayeachwa nyuma na hakabiliwi na hatari yoyote ya athari mbaya za polio," aliongeza.