Bush amuandikia baruwa kiongozi wa Korea Kaskazini
7 Desemba 2007Matangazo
WASHINGTON
Rais George W. Bush wa Marekani kwa mara ya kwanza kabisa ametowa wito binafsi kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Ill.
Katika baruwa Bush amemhimiza Kim kutangaza kikamilifu aina zote za nishati ya nuklea ya nchi hiyo na mipango yake ya silaha.
Serikali ya Korea Kaskazini imeahidi kukongowa mitambo yake ya nuklea iliozusha mzozo na kutowa ufafanuzi wa harakati zake zote za nuklea kufikia mwishoni mwa mwaka huu.