1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMisri

CAF: Al Ahly yaifunga Wydad Casablanca

5 Juni 2023

Mabao ya wachezaji Percy Tau na Mahmoud Kahraba yaliupatia ushindi klabu ya Misri ya Al Ahly

Ägypten | CAF Champions League 2022/23 | Finale – Al Ahly gegen Wydad
Picha: Weam Mostafa/Sports Inc/empics/picture alliance

Mabao 2-1 dhidi ya mabingwa watetezi Wydad Casablanca katika mkondo wa kwanza wa mechi ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika jana Jumapili.

Kunako dakika ya 86 ya mchezo, Saifeddine Bouhra aliifungia Wydad bao lao la pekee kwenye mchezo huo.

Soma pia: CAF yatangaza mfumo mpya wa kufuzu kombe la dunia 2026

Ushindi huo mwembamba unaipa nafasi ndogoAl Ahly ya kushinda kombe hilo kuelekea mechi ya mkondo wa pili Jumapili ijayo itakayochezwa ugenini.

Wachezaji wa Wydad Casablanca ya Morocco, walionekana kuridhika na matokeo hayo, kutokana na rekodi yao nzuri wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Sultan Mohammed wa tano (V) mjini Casablanca, ambapo waliipiga Al Ahly 2-0 na kushinda Kombe hilo katika fainali ya mwaka jana.

 Soma pia: Al Ahly yatamba Dar-es-salaam mbele ya Young Africans.

Waandalizi wa mashindano hayo wameamua kurejelea mfumo wa mikondo miwili ya fainali, ambao ulikuwa mfumo wa jadi kabla ya kufanyiwa mageuzi katika msimu wa mwaka 2019-20.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW