1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
KandandaTanzania

CAF: Michuano ya AFCON 2027 itafanyika kama ilivyopangwa

14 Februari 2026

Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika, Patrice Motsepe amesema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2027 itafanyika kama ilivyopangwa nchini Tanzania, Uganda na Kenya.

Algeria Algier 2022 | Mkutano na waandishi wa habari | Rais wa CAF- Patrice Motsepe
Rais wa Shirikisho la Soka la Afrika, CAF Patrice Motsepe amesema michuano ya AFCON 2027 itafanyika kama ilivyopangwa, Tanzania, Kenya na UgandaPicha: Wu Tianyu/Xinhua/IMAGO

Motsepe amesema hayo alipozungumza baada ya mkutano na kamati kuu ya CAF na kuongeza kuwa michuano hiyo itacheza mwezi Juni na Julai na shirikisho litatangaza tarehe ya kuanza hivi karibuni.

Motsepe ameyasema hayo baada ya mkutano na kamati kuu ya Shirikisho la Kandanda barani Afrika (CAF). Shirikisho hilo la Kandada litatangaza tarehe ya kuanza michuano hiyo hivi karibuni ambayo itachezwa mwezi Juni na Julai.

Michuano ya AFCON 2027 ambayo inaandaliwa na mataifa hayo matatu huenda ingesogezwa mbele hadi 2028.  

Katika mkutano huo Motsepe ameisifu Morocco iliyokuwa mwenyeji wa michuano hiyo mwaka 2025, na pia itakuwa mwenyeji wa AFCON kwa wanawake mwezi ujao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW