1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAF: Waliozusha vurugu fainali ya AFCON kuadhibiwa

19 Januari 2026

Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF limetoa kauli nzito likisema litachukua "hatua" dhidi ya watakaopatikana na hatia” kufuatia vurugu na hali ya sintofahamu zilizotokea wakati wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Kombe la Afrika 2025 | Finali | Senegal vs. Morocco |
Senegal yasherehekea ushindi wa AFCON uwanjani Prince Moulay Abdellah mjini Rabat Morocco mnamo Januari 18, 2026Picha: Siphiwe Sibeko/REUTERS

Kupitia taarifa rasmi, CAF imesema inalaani vikali tabia isiyokubalika iliyoonyeshwa na baadhi ya wachezaji na maafisa wakati wa fainali ya jana Jumapili. Taarifa hiyo imeongeza kuwa michuano ya AFCON inapaswa kuwa mfano wa nidhamu, heshima na ushindani wa kiungwana, na kwamba vitendo vinavyokiuka maadili hayo haviwezi kuvumiliwa.

CAF imeweka msisitizo juu ya uchunguzi wa kina na kuchukua hatua dhidi ya wahusika binafsi, iwe ni wachezaji, maofisa wa benchi la ufundi au viongozi wa timu

Katika fainali hiyo iliyochezwa mjini Rabat, wachezaji wa Senegal waliondoka uwanjani kama ishara ya kupinga uamuzi wa refarii Jean-Jacques Ndala baada ya kuwapa wenyeji Morocco penalti katika dakika za mwisho za muda wa nyongeza, wakati mchezo ukiwa bado 0-0.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW