1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cairo. Polisi wa Misr wapambana na watu wenye silaha katika msako.

25 Julai 2005

Polisi wa Misr wamefyatuliana risasi na watu wenye silaha leo wakati wakiwatafuta Wapakistani sita wanaotuhumiwa kuhusika katika mashambulio ya mabomu katika mji wa kitalii wa Sharm el – Sheikh ulioko ukingoni mwa bahari ya Sham.

Mashambuliano hayo na watu wa kabila la Bedouin yalizuka katika eneo la milimani la rasi ya Sinai kiasi cha kilometa 30 kutoka katika eneo ambalo lilishambuliwa kwa mabomu siku ya Jumamosi.

Mapambano hayo yalitokea baada ya polisi kuvizingira vijiji vya Khurum na Rweissat katika msako uliofanyika wakati wa usiku.

Duru za kiusalama zinasema kuwa , Wapakistan wawili walikuwa wakiishi katika eneo hilo na inasadikiwa kuwa mabomu yaliyolipuliwa yalitengenezwa hapo.

Polisi wa Misr wanawatafuta Wapakistan sita ikiwa ni sehemu ya uchunguzi kuhusika na mashambulizi ya mabomu dhidi ya mji wa kitalii wa Sharm el – Sheikh siku ya Jumamosi. Polisi wamesambaza picha za watu hao sita , ambao wametoweka tangu mabomu hayo kulipuka.

Wakati huo huo mabomu mawili ya kujitoa muhanga katika magari katika mji mkuu wa Iraq , Baghdad umesababisha watu 15 kuuwawa na karibu watu wengine 30 wamejeruhiwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW