SiasaAsia
Cambodia na Thailand zaendelea kushambuliana
13 Desemba 2025
Matangazo
Katika chapisho kwenye mtandao wa Facebook, wizara ya ulinzi ya Cambodia imesema vikosi vya Thailand bado havijasitisha mashambulizi yake.
Kwa upande wake, jeshi la Thailand liliandika kwenye X kwamba Cambodia ilirusha makombora kwenye maeneo ya kiraia katika mkoa wa Sisaket, na kuwajeruhi raia wanne.
Waziri Mkuu wa Thailand Anutin Charnvirakul, pia ameviambia vyombo vya habari vya ndani kwamba hakukuwa na usitishaji mapigano katika mzozo huo wa mipaka.
Baada ya mawasiliano na Trump, Anutin aliwaambia waandishi wa habari huko Bangkok kwamba lazima Cambodia iwe ya kwanza kusitisha mapigano.
Amesema upande uliokiuka makubaliano ya kusitisha mapigano ndio unaopaswa kurekebisha mienendo yake na wala sio ulioushambuliwa.