Mchezaji soka wa zamani wa Cameroon ameanzisha mradi wa matumizi mapya ya mabaki ya plastiki. Roger Milla tayari ameshaweka jiwe la msingi mji mkuu wa Younde la kiwanda kitakachotengeneza mawe pamoja na bamba za kujengea njia za waendao kwa miguu kwa kutumia mchanganyo wa plastiki pamoja na mchanga.