1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cameroon yatangaza siku ya maombolezo ya kitaifa

29 Oktoba 2020

Rais wa Cameroon Paul Biya ametangaza kwamba Jumamosi itakuwa siku ya maombolezo baada ya wanamgambo wasiojulikana waliokuwa na silaha kuwauwa watoto saba katika shambulio lilotokea shule moja nchini humo

Kamerun Präsident Paul Biya
Picha: picture-alliance/AP Photo/S. Alamba

Mbali na mauaji hayo, watoto wengine 13 wamejeruhiwa vibaya baada ya wanamgambo hao kuwafyatulia risasi wanafunzi wa shule ya Mother Francisca katika mji wa Kumba wa eneo la Cameroon linalozungumza lugha ya Kiingereza.Biya amesema jana kuwa amesikitishwa sana na mauaji hayo na ameamrisha kufanyika uchunguzi wa kina wa shambulio hilo.

Hadi hivi sasa hakuna kundi lilodai kuhusika na shambulio hilo. Lakini katika siku chache zilizopita, maafisa wa serikali na wapiganaji wa makundi yanayotaka kujitenga yamekuwa yakinyosheana kidole cha lawama kuhusiana na shambulio hilo.Cameroon imetumbukia katika machafuko tangu mwaka 2016, pale maeneo mawili ya Kaskazini-Magharibi na Kusini-Magharibi yanayozungumza Kiingereza kutangaza kutaka kujitenga mbali na kuunda nchi yao mpya itakayoitwa  Ambazonia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW