1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CANADA KUPIGANIA MIKATABA YA UJENZI-IRAQ:

14 Januari 2004

MONTERREY: Rais George W.Bush wa Marekani amesema makampuni ya Canada yataruhusiwa kuzabunia mikataba juu ya ujenzi wa Iraq katika duru ya pili ya kutolewa mikataba hiyo.Mwezi uliopita,ikitoa sababu za usalama wa taifa,serikali ya Washington ilisema mikataba muhimu itatolewa tu kwa zile nchi zilizounga mkono vita dhidi ya Iraq.Waziri mkuu wa Canada Paul Martin amefurahia msimamo huu mpya wa Marekani.Viongozi hao wawili walikutana pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Nchi za Amerika,uliofanywa Monterrey nchini Mexico.Canada iliokuwa ikiongozwa na waziri mkuu wa zamani Jean Chretien ilikataa kuunga mkono uvamizi wa Iraq ulioongozwa na Marekani.Bush hakusema ikiwa nchi zingine pia zilizopinga vita,kama vile Ujerumani na Ufaransa,zitaruhusiwa wakati wa duru ya pili kupigania mikataba ya ujenzi wa Iraq.