1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaCanada

Canada yaomba radhi baada ya kumsifu aliyehudumu na Nazi

28 Septemba 2023

Waziri Mkuu wa Canada amesema kumwalika mwanajeshi raia wa Ukraine aliyepigana Vita vya Pili vya Dunia, ambaye baadae ilitambulika kwamba alihudumu pamoja na utawala wa Nazi, lilikuwa ni kosa la "aibu".

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema ni aibu kubwa kumsifia hadharani mtu aliyehusika na uhalifu chini ya utawala wa Nazi
Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema ni aibu kubwa kumsifia hadharani mtu aliyehusika na uhalifu chini ya utawala wa NaziPicha: Sean Kilpatrick/The Canadian Press/AP/picture alliance

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau ameomba radhi baada ya wabunge kumsifia hadharani mtu aliyehudumu katika utawala wa Nazi, wakati rais Volodymyr Zelensky alipokuwa akitoa hotuba wiki iliyopita.

Mwanajeshi huyo Yaroslav Hunka aliyepigana Vita vya Pili vya Dunia na raia wa Ukraine alijulikana kuhudumu katika Kitengo cha kijeshi cha Nazi cha Waffen-SS Galicia, ambacho ni miongoni mwa vitengo vilivyofanya uhalifu dhidi ya ubinadamu wakati wa mauaji ya Wayahudi.

Trudeau amemuomba radhi rais Zelensky kufuatia tukio hilo la Ijumaa, pamoja na ujumbe wa Ukraine akizingatia hisia zao kutokana na tukio hilo.

Amesema kumtambua mtu huyo bila kujua, lilikuwa ni kosa kubwa na ukiukaji wa kumbukumbu ya wale walioteseka mikononi mwa serikali ya Nazi. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW