SiasaCanada
Canada kuwa tayari kujibu hatua ya Trump kuhusu ushuru
16 Januari 2025Matangazo
Hata hivyo Waziri Mkuu huyo wa Canada amesisitiza kuwa na matumaini ya kuepusha vita vya kibiashara. Baada ya kukutana na viongozi wa majimbo na wilaya huko Ottawa, Trudeau amesisitiza kuwa zaidi ya dola bilioni moja zimetengwa ili kuidhinisha hatua mpya za usalama wa mpakani ili kudhibiti biashara haramu ya dawa za kulevya na usafirishaji wa binadamu.
Trump anayetarajia kuapishwa rasmi Januari 20, ameapa kuidhinisha ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa zote zinazoingia Marekani kutokea Canada . Trudeau amesisitiza kuwa ikiwa Marekani itaidhinisha ushuru huo, watajibu kwa nguvu na kwa uthabiti.