1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Canberra: Australia imewatahadharisha wananchi wake wasizitembelea Kenya,...

3 Desemba 2003
Pakistan na Afghanistan.Chanzo cha onyo hilo ni kitisho cha kuzuka wimbi la mashambulio ya kigaidi.Taarifa ya wizara ya mambo ya nchi za nje mjini Canberra inazungumzia juu ya ripoti za kuzuka wakati wowote ule kutoka sasa mashambulio ya kigaidi dhidi ya hoteli za kimataifa mjini Nairobi.Nchini Pakistan hujuma za kigaidi zinahofiwa kutokea katika mji wa bandari wa Karachi.Hali ya tahadhari imetangazwa pia nchini Malaysia ambako magaidi toka nchi jirani ya Philipiines wanatuhumiwa kuandaa mashambulio dhidi ya vituo vya kibiashara na eneo la kuvutia watalii Sabah katika kisiwa cha Borneo.Australia kila kwa mara imekua ikiwasihio wananchi wake watahadhari kufuatia shambulio la kigaidi la Bali nchini Indonesia october mwaka jana ambapo watu 202 waliuwawa.88 kati ya wahanga wa shambulio la Bali walikua raia wa Australia.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW