CANBERRA:Sheria kali za kudhibiti ugaidi zatangazwa nchini Australia.
8 Septemba 2005Matangazo
Waziri Mkuu wa Australia,John Howard ametangaza hatua kali za kisheria kupambana na vitendo vya kigaidi.
Sheria hiyo mpya sasa itawapa uwezo askari polisi kutumia njia za kielektroniki,kufuatilia nyendo za watuhumiwa wa kigaidi kwa kipindi hadi cha mwaka mmoja,kuongeza uwezo wa kuwaweka kizuizini watuhumiwa,na sheria kali za kudhibiti wageni.
Bwana Haoward amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kutokea mashambulio ya mabomu mjini London,Uingereza yaliyoendeshwa na Waislamu raia wa Uingereza mwezi wa Julai,ambapo watu zaidi ya 50 waliuawa na pia mtazamo uliopo kuwa Australia nayo inanyemelewa na mashambulio ya aina hiyo.