CAPE TOWN: Afrika Kusini itakuwa na kiti katika Baraza la Usalama
6 Septemba 2006Matangazo
Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini amesema, kuanzia mwakani nchi yake,itakuwa na kiti katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kama mwanachama wa muda kwa kipindi cha miaka mwili.Mbeki,alitoa tangazo hilo baada ya mazungumzo yake pamoja na rais wa Urussi,Vladimir Putin mjini Cape Town.Putin anafanya ziara ya siku mbili nchini Afrika Kusini.Hiyo ni ziara ya kwanza kupata kufanywa na kiongozi wa Kirussi nchini Afrika Kusini.Mbali na mikutano yake pamoja na Mbeki na viongozi wengine,Putin atashuhudia pia kutiwa saini kwa mikataba ya uwekezaji wa Urussi katika sekta za migodi,almasi na vyuma.