1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAPE TOWN : Waziri wa afya asusia mkutano wa UKIMWI

6 Juni 2007

Waziri wa Afya wa Afrika Kusini Manto Tshabalala –Msimang ameususia mkutano wa taifa wa UKIMWI leo hii wakati akirudi kazini kufuatia operesheni ya kupandikizwa ini.

Waziri huyo alikuwa akitarajiwa kuhutubia mkutano huo katika mji wa mwambao wa Durban lakini amejitowa baada ya waandalizi wa mkutano huo kumpa nafasi zaidi ya kuzungumza naibu wake ambaye ana mahusiano mazuri zaidi na wanaharakati wa UKIMWI kuliko yeye.

Tshabalala-Msimang amebebeduliwa duniani kote kutokana na kutetea matumizi ya kitunguu thomu,mboga aina ya beetroot na mafuta ya alizeti kutibu virusi vya HIV na UKIMWI.

Waziri huyo amepangwa kuhutubia jopo moja tu.

Mkutano huo unatarajiwa kufikia muafaka mpya katika sera za UKIMWI nchini Afrika Kusini ambazo zimekuwa zikikwamishwa kutokana na mfarakano na kutafautiana juu ya namna ya kupambana na gonjwa hilo thakili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW