CARACAS: Venezuela yamrejesha nyumbani balozi wake
4 Agosti 2006Matangazo
Rais Hugo Chavez wa Venezuela amesema amemuita nyumbani balozi wake kutoka Israel,kama ishara ya kupinga mashambulio ya kijeshi yanayofanywa Lebanon na katika Ukanda wa Gaza.Katika hotuba yake iliyotangazwa kwenye televisheni,Chavez ameyaita mashambulio ya Israel nchini Lebanon “mauaji ya halaiki”.Chavez,anaejulikana kama ni mkosoaji mmojawapo mkuu wa Marekani,ametoa mwito kwa Umoja wa Mataifa kusitisha mapigano nchini Lebanon.Chavez ambae serikali yake hadi hivi sasa imesema ina uhusiano mzuri na Israel,akaongezea kuwa amehamakishwa na mashambulio ya Israel ambayo huungwa mkono na Marekani.