1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Casablanca, Morocco. Wahamiaji warejeshwa nyumbani.

14 Oktoba 2005

Morocco imewarejesha nyumbani Waafrika kadha wengine, wakitumia ndege tatu kuwarejesha wahamiaji hao jana Alhamis.

Morocco ilianza kuwarejesha watu hao kutoka mataifa yaliyoko kusini mwa jangwa la Sahara mapema wiki hii, kufuatia ongezeko la wimbi la hivi karibuni la watu hao kujaribu kuingia katika matiafa ya umoja wa Ulaya kupitia maeneo yanayomilikiwa na Hispania katika pwani ya kaskazini ya Morocco.

Waafrika 11 wameuwawa katika wiki za hivi karibuni wakati wakijaribu kupanda uzio wa waya katika maeneo ya Melilla na Ceuta.

Mawaziri wa sheria wa umoja wa Ulaya walikutana siku ya Jumatano kuangalia njia za kulishughulikia suala hilo la wahamiaji haramu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW