1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Casillas alijiunga na Real Madrid akiwa na umri wa miaka 9

4 Agosti 2020

Mlinda lango wa zamani wa timu ya taifa ya Uhispania na Real Madrid Iker Casillas amethibitisha kustaafu soka

Fußball-WM 2010 - Weltmeister Spanien Gerard Pique
Picha: picture-alliance/dpa/B. Weissbrod

Kupitia ukurusa wake wa kijamii wa Facebook, Casillas mwenye umri wa miaka 39 amesema ametimiza ndoto yake ya soka.

Mlinda lango huyo ameshinda mataji mawili ya kombe la Ulaya pamoja na kombe la dunia akiwa na timu ya taifa ya Uhispania.

Vile vile, ameshinda mataji matano ya ligi kuu ya Uhispania La Liga na kombe la bara Ulaya Champions League mara tatu akiwa na Real Madrid.

Hata hivyo, Casillas hajaichezea mechi yoyote klabu yake ya Porto tangu alipopata mshtuko wa moyo mnamo Mei 1, 2019. Kwa wakati huu zipo tetesi kuwa Real Madrid inanuia kumrejesha klabuni humo ili awe kama balozi.

Jarida la michezo la Marca limemtaja Casillas kama mlinda lango bora katika historia ya soka la Uhispania.

Casillas amecheza mechi 1,039 na kushinda mataji 24.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW