1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CCM kushinda uchaguzi mkuu wa Tanzania

10 Mei 2005

Zanzibar:

Rais wa Tanzania anayeng’atuka, Benjamin Mkapa, ametabiri kuwa chama chake tawala cha CCM kitashinda kwa wingi mkubwa katika uchaguzi mkuu ujao wa Oktoba 30 mwaka huu. Rais Mkapa amesema hayo wakati alipokuwa anahutubia halaiki ya watu kisiwani Zanzibar akifanya kampeni ya kuungwa mkono Wagombea wa Chama cha Mapinduzi. CCM, juma lililopita, imemchagua Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania, Jakaya Kikwete, kugombea urais na mgombea wake mwenzi ni Makamu wa Rais Ali Mohamed Shein. Rais Mkapa, kwa mujibu wa katiba, haruhusiwi kugombea kipindi kingine cha tatu. Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar amechaguliwa na CCM kugombea tena wadhifa huo kwa kipindi cha pili. Kwa mujibu wa katiba, Zanzibar ina haki ya kumchagua Rais wake na Wabunge.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW