1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CDC: Afrika inakabiliwa na milipuko mingi ya kipindupindu

14 Novemba 2025

Kituo cha kudhibiti magonjwa ya milipuko barani Afrika-Africa CDC kimetangaza kwamba kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 25 iliyopita bara la Afrika linakabiliwa na milipuko mingi ya ugonjwa wa kipindupindu.

Sudan Tawila 2025 | Mgonjwa wa kipindupindu
Mgonjwa wa Kipindupindu akisubiri matibabu Sudan.Picha: Mohammed Jamal/REUTERS

CDC imeyatangaza hayo mjini Addis Ababa Ethiopia katika kikao na waandishi wa habari huku ikitaja kuwa chanzo cha tatizo hilo ni mizozo inayoendelea barani Afrika lakini pia mifumo hafifu ya kuhifadhi na kutunza mifumo ya maji katika makazi ya watu. 

Kituo hicho cha CDC kimesema kwamba tayari watu elfu saba barani Afrika wameshapoteza maisha yao kutokana na ugonjwa wa kipindupindu huku vikirikodiwa visa vingine mia tatu vya ugonjwa huo. Idadi hiyo ya vifo CDC inasema inaonyesha ongezeko la asilimia 30% ya vifo kama hivyo ndani ya mwaka uliopita

CDC pia imesema kwamba nchi za Angola na Burundi zimeathirika zaidi kwa wiki za hivi karibuni ambapo sababu kubwa ya ongezeko hilo katika nchi hizo ni pamoja na mifumo mibovu ya maji safi na salama kwa wananchi.

Kituo hicho kimesema ugonjwa wa kipindupindu ni hatari na ni mkali sana kutokana na kusambaa kwa haraka endapo mifumo ya maji taka na maji ya matumizi ya nyumbani vinapokuwa havitunzwi vizuri ipasavyo.

Hata hivyo mlipuko wa magonjwa hayo ambao awali ulikuwa ukiripotiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umeendelea kudhibitiwa inapasavyo hali ambayo sasa inaonekana kusaidia kupunguza kiwango cha kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa huo nchini humo.

CDC: Maeneo ya mizozo inaathirika zaidi

Taarifa ya CDC inaonyesha maambukizi ya kipindupindu yanaonekana kusambaa kwa kasi katika maeneo yenye mizozo na vita na hali hii inaendelea kusababisha hali ya wasiwasi wa maambukizi zaidi hasa katika kambi za wakimbizi ambapo kuna msongamano wa makazi na watu huku mfumo wa maji safi na salama ukiwa hautoshi.

Wahudumu wa afya Sudan wakiwahudumia wagonjwa wa kipindupunduPicha: Mohammed Jamal/REUTERS

Lakini kwa upande mwingine nchi za Somalia na Sudan Kusini pia zimeonekana kuendelea kufanya vizuri kwa sababu awali zilisumbuliwa na milipuko ya ugonjwa huo.

Dr Jean Kaseya mkurugenzi mkuu wa CDC Africa amesema na hapa namnukuu  amesema kwamba kipindupindu bado ni tatizo kubwa, ni kana kwamba kila mwaka tuna ongezeko la maambukizi ya ungojwa huu,huku akisisitiza  bila maji safi na salama ugonjwa huu hauwezi kukomeshwa 

Dr Kaseya amesema kila mwaka bara la Afrika linahitaji chanjo milioni 54 za ugonjwa wa kipindupindu lakini zinazopatikana ni nusu ya kiasi hicho suala ambalo linaendelea kuyaweka hatarini maisha ya waafrika wengi, akasema hilo ni suala lisilokubalika huku akizitaka nchi za kiafrika kuharakisha mchakato wa kutengeneza chanjo barani Afrika.

Lakini katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres akiwahutubia viongozi wa Afrika mapema wiki aliutaka ulimwengu ulioendelea kutoipa kisogo Afrika

"Dunia haitakiwi kuipa mgongo Afrika, sehemu ambako kunaishi karibu asilimia ishirini ya binadamu wote, hii ni sehemu kubwa na ustawi ni mkubwa mno"

Kituo hicho cha CDC kimesema pia kwamba nchi ya Ethiopia imerekodi visa vinane vya homa kali ya mlipuko ambayo bado haijatambuliwa lakini kwamba uchunguzi wa kina na wa mara moja umeanza kuweza kudhibiti mlipuko huo.

Katika maeneo mbalimbali barani afrika pia janga la ugonjwa wa Mpox ambao hapo awali ulisadikiwa kuuawa idadi ya watu wengi nchini Tanzania na maeneo mengine sasa umedhibitiwa.

Hata hivyo CDC linasema linaendelea kufuatilia kwa ukaribu nchi kama Kenya, Guinea, Liberia na Ghana ambako kuna uwezekano wa kuripuka upya kwa ugonjwa huo.

Changamoto ya utiririshaji wa maji taka Dar es Salaam

02:21

This browser does not support the video element.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW