1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CDC yathibitisha mlipuko wa Ebola nchini Kongo

15 Mei 2026

Mlipuko mpya wa ugonjwa hatari wa homa ya Ebola umethibitishwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na tayari umesababisha vifo vya watu 65 na wengine karibu 250 wanashukiwa kuwa wameambukizwa.

Udhibiti wa Ebola
Ugonjwa wa Ebola husambazwa kwa binadamu kutoka jamii ya popo walao matunda. Picha: Luke Dray/Getty Images

Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa na Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa barani Afrika, CDC, ambacho kimesema visa vya mwanzo vimeripotiwa kwenye jimbo la Ituri.

CDC imesema inafuatilia kwa karibu mlipuko huo na inasaidia utayari wa kukabiliana na kusambaa zaidi ugonjwa huo ndani ya Kongo pamoja na kwenye mataifa jirani.

Ugonjwa wa Ebola uliogunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1976 hutokana na virusi vinavyosambazwa na jamii fulani ya popo walao matunda.

Ugonjwa huo ambao husababisha mgonjwa kuvuja damu na athari kwenye viungo muhimu vya mwili umewaua zaidi ya watu 15,000 barani Afrika tangu ulipogunduliwa miaka 50 iliyopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW