1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CDU yaongoza katika uchaguzi wa North Rhine-Westphalia

15 Septemba 2025

Chama cha Christian Democratic Union, CDU, kinaongoza katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika jana katika jimbo la North Rhine-Westphalia (NRW) lililo na idadi kubwa ya watu hapa nchini Ujerumani.

Deutschland Düsseldorf 2025 | Friedrich Merz
Kansela wa Ujerumani Friedrich MerzPicha: Frank Ossenbrink/IMAGO

Matokeo ya awali yanaonyesha chama hicho cha Kansela Friedrich Merz kinatarajiwa kujizolea asilimia 33.3 ya kura kikifuatiwa na chama cha siasa za wastani zinazoegemea mrengo wa kushoto cha SPD kikiwa na asilimia 22.1 ya kura.

Chama kinachofuata siasa kali za mrengo wa kulia, AfD, kilichokuwa kinafuatiliwa kwa karibu na waagalizi wa uchaguzi huu kinatazamiwa kupata asilimia 14.5 ya kura.

Vyama vingine ikiwemo kile cha kijani (Die Grünne) na FDP vinatarajiwa kupata matokeo mabaya.

Uchaguzi wa jimbo la NRW, ambao ni wa kwanza tangu Merz alipoingia madarakani mwezi Mei, unaangaliwa kama kipimo kwa serikali yake ya muungano. Kansela huyo alisema atafuatilia matokeo ya uchaguzi huu kwa makini kujua kile wapiga kura wanachokitaka katika siasa za kikanda na kitaifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW