CEUTA: Ziara ya mfalme Juan Carlos yazusha hisia kali
6 Novemba 2007Matangazo
Serikali ya Morroco imekasirishwa na ziara ya mfalme Juan Carlos wa Uhispania katika sehemu ya Uhispania iliyo barani Afrika.
Mfalme Juan Carlos na malkia Sofia walikaribishwa kwa shangwe na maelfu ya Wahispania wanaoishi katika katika mji wa pwani wa Ceuta amabao Morroco unauchukulia kuwa ni sehemu ya nchi yake.
Waziri mkuu wa Morroco Abbas El Fassi ameikosoa ziara hiyo na kutoa mwito kwamba visiwa vya Ceuta na Melilla vinapaswa kurejeshwa mikononi mwa Morroco au kwa maneno mengine ni sehemu ya bara la Afrika.