1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chad yatangaza maombolezo ya kitaifa baada ya shambulio

7 Mei 2026

Serikali ya Chad katika taarifa yake imetangaza maombolezo ya kitaifa ya hadi siku ya Jumamosi Mei 9 kuwaenzi wanajeshi hao. Hiyo ni kufuatia kuuliwa kwa wanajeshi wengine wawili hapo jana na Boko Haram.

Tschad Tine 2025 | Soldaten kontrollieren Fahrzeuge am Grenzposten zu Sudan
Wanajeshi wa Chad wakiwa kwenye ukaguzi Picha: Amr Abdallah Dalsh/REUTERS

Chad imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa baada kuuliwa kwa majenerali wawili katika ufuo wa Ziwa Chad kwenye shambulio jipya lililofanywa na wanamgambo wa kundi la Boko Haram.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi ni kwamba siku ya Jumatatu jioni, shambulio katika kambi ya kijeshi ya Barka Tolorom kwenye ufuo wa Ziwa Chad liliwaacha wanajeshi wasiopungua 24 wakiwa wamekufa na kadhaa kujeruhiwa.

Alasiri siku ya Jumatano, boti za usalama na vikosi vya ulinzi vilivyokuwa vikishika doria katika eneo hilo "ziliangukia tena katika shambulio lingine la Boko Haram," hayo yamesemwa na afisa mmoja wa jeshi alipozungumza na shirika la habari la AFP, akiongeza kuwa majenerali wawili waliuawa.

Serikali ya Chad katika taarifa yake imetangaza maombolezo ya kitaifa ya hadi siku ya Jumamosi Mei 9 kuwaenzi wanajeshi hao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW