1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChad

Chad yafanya uchaguzi wa bunge na serikali za mitaa

29 Desemba 2024

Raia wa Chad leo wanashiriki uchaguzi wa bunge na wa serikali za mitaa baada ya miaka mitatu ya utawala wa kijeshi.

Chad | Uchaguzi
Watu wa makabila ya kuhamahama ya Chad kutoka eneo la Ati wanapiga kura katika uchaguzi wa bunge na serikali za mitaa katika kituo cha kupigia kura eneo la Mandelia.Picha: Joris Bolomey/AFP

Uchaguzi huo umetajwa na serikali kama hatua ya mwisho ya mpito wa kisiasa, baada ya miaka mitatu ya utawala wa kijeshi.

Hata hivyo upinzani umeususia uchaguzi huo ukipinga kile unachokiita ‘mfumo uliojengwa kwenye misingi ya uongo na wizi wa kura'.

Soma pia: Kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa kunawatia wasiwasi Wachad 

Kupitia ukurasa wa Facebook, upinzani umewataka wafuasi wao kutojitokeza ukisema matokeo ya uchaguzi huo tayari yapo kwenye makompyuta hata kabla ya kura kupigwa.

Hatua ya upinzani kususia uchaguzi huo imewaacha wagombea wanaoegemea upande wa Rais Mahamat Idriss Itno bila ushindani.

Jenerali Mahamat Idriss Itno, aliwekwa madarakani na jeshi mnamo mwaka 2021 na kisha kushinda katika uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi Mei mwaka jana ambao wagombea wa upinzani waliukosoa kuwa ulikumbwa na udanganyifu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW