1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chad yafanya uchaguzi baada ya miaka 3 ya utawala wa kijeshi

30 Desemba 2024

Raia wa Chad walipiga kura hapo jana katika uchaguzi mkuu ambao serikali imeusifu kuwa ni hatua muhimu ya mpito wa kisiasa, baada ya miaka mitatu ya utawala wa kijeshi.

Wahlkampagne in Tschad
Meya wa N'Djamena na na watu wengine wakiwa kwenye mkutano wa kampeni ya Patriotic Salvation Movement (MPS) katika wilaya ya Sabangali ya N'Djamena, Desemba 14, 2024.Picha: Joris Bolomey/AFP

Hata hivyo uchaguzi huo ulishuhudia idadi ndogo ya wapiga kura huku upinzani ukitoa wito wa kuususia kutokana na madai ya udanganyifu. Rais Mahamat Idriss Deby Itno, alichukua madaraka mwaka wa 2021 baada ya kifo cha babake, ambaye alikuwa ameiongoza nchi hiyo kwa miongo mitatu na kisha kushinda katika uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi Mei mwaka jana ambao wagombea wa upinzani waliukosoa kuwa ulikumbwa na udanganyifu. Kiongozi wa chama cha upinzani cha Transformers amesema wapiga kura walisikia mwito na wengi wao wakasalia majumbani mwao. Vituo vya kupigia kura vilifuatiliwa na karibu waangalizi 100 wa kigeni na wawakilishi wa vyama vya kisiasa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW