SiasaChad
Chad yasema shambulio lililotibuliwa lilifanywa na walevi
9 Januari 2025Matangazo
Milio ya risasi ilisikika karibu na ofisi ya rais katika mji mkuu, N'djamena Jumatano usiku huku jeshi likishika doria na kufunga barabara.
Serikali ilisema baadaye kuwa, vikosi vya usalama vilizuia jaribio la kile walichokiita kudhoofisha nchi hiyo ya Afrika ya Kati na kwamba hali kwa wakati huu imedhibitiwa kabisa.
Katika mahojiano kwenye televisheni ya taifa, msemaji huyo wa serikali ya Chad ameeleza kwamba kundi la washambuliaji 24 waliokuwa na visu na mapanga na waliokuwa walevi, walijaribu kuivamia ikulu ya rais.
Amesema kuwa, washambuliaji hao waliwavamia walinzi wanne waliokuwa kwenye lango la ikulu, na kumuua mlinzi mmoja na kuwajeruhi wengine wawili.