1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiChad

Chad yatoa tahadhari ya mafuriko mabaya zaidi

Saleh Mwanamilongo
5 Oktoba 2024

Hali hiyo imekuja wakati ambapo nchi hiyo inapitia kipindi kigumu kujinasua kutoka kwenye mafuriko mabaya yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 500.

Serikali ya Chad yatoa tahadhari ya mafuriko zaidi baada ya mito miwili kufurika
Serikali ya Chad yatoa tahadhari ya mafuriko zaidi baada ya mito miwili kufurikaPicha: Mahamat Ramadane/REUTERS

Kulingana na Waziri Mkuu Allamaye Halina, mto Chari umefurika mita nane zaidi ya kiwango chake katika kipindi cha siku kumi zilizopita.

Mafuriko hayo makubwa huko Chad ambayo yamekuwa yakishuhudiwa tangu Julai, tayari yamewaathiri zaidi ya watu milioni 1.7, kuharibu nyumba laki moja na sitini na nne elfu na ekari laki mbili na hamsini elfu za mashamba.

Mafuriko hayo vile vile yamewazamisha ng'ombe sitini elfu wakati ambapo kila mkoa nchini humo umeathirika. Mvua kubwa katika eneo hilo la Afrika magharibi na kati imesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu moja miatano katika nchi za Chad, Nigeria, Cameroon, Burkina Faso na Guinea.