1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chadema kususia mchakato wa kurekebisha sheria za uchaguzi

10 Novemba 2022

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema, kimesema hakitashiriki katika mchakato wa marekebisho ya sheria za uchaguzi na sheria ya vyama vya siasa.

Chadema Chairman Freeman Mbowe
Picha: Ericky Boniphace/DW

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema kimesema hakitashiriki katika mpango utakaoendeshwa na Tume ya kurekebisha sheria iliyoko chini wizara ya katiba na sheria ambayo imepanga kuanzia kesho kuzunguka nchi nzima kukutana na wadau mbalimbali ikiwamo vyama vya siasa kwa ajili ya kuanzisha mchakato wa marekebisho ya sheria za uchaguzi na sheria ya vyama vya siasa.

Chadema katika tamko lake leo kuhusiana na  jambo hilo, imepinga hatua hiyo ikitaka isitishwe mara moja ikisisitiza imetoa maagizo kwa viongozi wake kote nchini.

Moja ya mambo iliyotaja ni kwamba haiwezekani kuanzishwa mchakato wa marekebisho ya sheria za uchaguzi bila kwanza kuwa na tume huru ya uchaguzi.

Kwa maoni ya chama hicho masuala tete yanayozuliwa na katiba kama vile kukosekana kwa tume huru, kutohojiwa mahakamani matokeo ya urais, ni masuala yaliyopaswa kwanza kushughulikiwa kabla ya  mengine kuanzishwa.Picha: Ericky Boniphace/DW

Chadema yakosoa bima ya afya kwa wote

Akitoa msimamo wa chama, Katibu mkuu wa chama hicho, John Mnyika amesema ni jambo linalopingana na ukweli wa mambo kuanzisha mchakato wa mapitio ya marekebisho ya sheria za uchaguzi na vyama vya siasa, wakati mzizi wa tatizo bado haujashughulikiwa.

Hatua ya tume ya kurekebisha sheria kuanzisha mchakato wa mapitio ya marekebisho ya sheria za uchaguzi na za vyama vingi inakuja siku chache baada ya timu iliyokulikana kama kikosi kazi kilichoratibu masuala ya demokrasia kukabidhi ripoti yake kwa Rais.

Chadema kususia mchakato wa kurekebisha sheria za uchaguzi

This browser does not support the audio element.

Chadema chamshitumu rais Samia kwa uvunjifu wa Katiba na sheria

Lakini Chadema inasisitiza kuwa, hatua inayochukuliwa sasa haitoa mustakabali mwema juu ya hatma ya vyama vya saisa ikidai pia pengine itazidi kuipa nguvu  ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kuwa na usemi zaidi dhidi ya vyama hivyo.

Chama hicho mbali ya kuweka msimamo huo, kimehoji pia namna tume ya marekebisho ya sheria ilivyoendelea kuwa kimya juu ya marufuku ya vyama vya siasa kufanya mikutano yake ya hadhara ilihali ikielezwa kuwa mikutano hiyo imewekwa kisheria.